Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 4 September 2015

HATARII!! HAYA NDIYO MADHARA AMBAYO UNAWEZA KUYAPATA ENDAPO UKITOA MIMBA


Habari za leo Ijumaa ya Septemba 04, 2015 mdau wa www.dkmandai.com karibu tena tuendelee kukufahamisha yale ambayo Mwenyezi Mungu atakuwa amejalia tukufikishie kwa leo.


Kuna swali lilitumwa na mfuatiliaji wa Mandai Herbalist Clinic ambaye yeye liomba kufahamu madhara ambayo huweza kumkuta mwanamke aliyetoa mimba.

Nami nikaona si mbaya kama tukiamua kulijibu swali lake kwa faida yake pamoja na wengine wengi ambao wanafuatilia tovuti hii.

Kwa kuanza kwanza ni vyema ikafahamika kwamba kitendo cha kutoa mimba huweza kumsababishia mhusika madhara mbalimbali ikiwa ni pamoja kifo, mhusika kupoteza damu nyingi na maambukizi hatarishi katika mfuko wa uzazi au mirija ya uzazi.

Hata hivyo endapo mhusika atabahatika kufanikisha zoezi hilo bado atakumbwa na athari ngingine baadaye kama vile kusababisha uharibifu wa mfuko wa uzazi na huweza kuchangia mirija ya uzazi kubaki na makovu kwenye ile ngozi laini ya mfuko wa uzazi, jambo ambalo humsababishia maumivu makali mwaamke anapokaribia siku zake za hedhi ama kuupoteza mzunguuko wake.

Kutokana na kujifunga kwa mirija ya uzazi, athari ni kuwa mbegu ya yai la mwanaume ambayo ni ndogo hupata tabu ya kuingia, na mbegu ya yai la mwanamke ambayo ni kubwa hupita na yanapokutana kusabibisha mimba kutungwa nje ya kizazi na kwasababu mimba hiyo iko nje ya mazingira ya kawaida, inaweza ikapasuka na kupoteza damu nyingi na kusababisha kifo.

Madhara mengine anayoweza kuyapata mwanamke kwa kutoa mimba ni ugumba Hali hii inatokana na uharibifu wa mazingira ya mpango wa mfuko wa uzazi na hasa kwa uchokonoaji wa mimba, hivyo kufungwa kwa kizazi.

Tatizo hili la ugumba huwa linasababishwa na kukwanguliwa kwa ile ngozi laini inayozunguka tumbo la uzazi. Kukwanguliwa huko kunatokana na vifaa vinavyotumiwa kuichokonoa mimba hiyo au madawa makali.

Pia wanawake wanaotoa mimba wana hatari kubwa ya kupata saratani ya mlango wa uzazi kuliko wengine ambao hawajatoa mimba. Hii ni kwasababu ya kusumbuliwa kwa mlango huo kwa dawa za kutoa mimba na vifaa vya kutoa mimba.

Kimsingi ni kwamba utoaji wa mimba ni hatari sana na ni kinyume na sheria za nchi yetu, lakini pia hata Mwenyezi Mungu hapendezwi kabisa na tabia hiyo. Hivyo napenda kutoa ushauri kwa wanawake wote kuacha tabia hiyo mara moja na kuepuka kubeba mimba. 


Kwa ushauri unaweza wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment