Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 3 September 2015

HILI NDIO SWALI LA LEO KUTOKA KWA MWANANCHI WA KAWAIDA KWENDA KWA TABIBU MANDAI, YAPATE HAPA MAJIBU YAKE

Tabibu Abdallaha Mandai Mkurugenzi Mkuu wa Mandai Herbalist Clinic

Tabibu Abdallah Mandai kutoka Mandai Herbalist Clinic mara nyingi huwa anapokea maswali kwa namba zake za simu ambazo ni 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 kila siku .

Lakini asubuhi ya leo Septemba 03, 2015 kuna sms kadhaa ziliingia kwenye simu yenye namba 0769 400 800, sasa kati ya hizo sms kadhaa moja ya sms ilikuwa imeandikwa hivi "aisee  du hali si hali hivi kukoroma kunasababishwa na nini? nipe ushauri wako"

Tabibu Mandai anasema kwanza kabisa  tafsiri ya haraka aliyoipata mara baada ya kupata sms hiyo ilikuwa ni kwamba huenda mtu huyo aliyonitumia sms hiyo alikuwa amekwazika sana 'usiku' huenda kutokana na kulala na mtu mwenye shida hiyo ya kukoroma.

Hivyo kwa faida ya ndugu aliyenitumia sms hiyo na wasomaji wengine wa www.dkmandai.com napenda kulijibu swali hilo kama ifuatavyo:
 
Kukoroma ni tatizo linalowapata watu wengi wakati wanapolala ambalo linaweza kuwatokea watu wa kila umri ingawa hutokea mara nyingi kwa wanaume au watu wanene.
 

Tatizo hili mara nyingi huwapata zaidi watu wazima kuliko watoto. Hata hivyo hii si shida kubwa sana, lakini mara nyingi huleta tu karaha kwa mtu anayelala karibu na mkoromaji.
 

Tatizo hili hujitokeza pale mtu anapokuwa na kitu au sababu yoyote itakayoziba kuingia au kutoka kwa hewa mdomoni na katika pua. Hivyo kuta za koo hutikisika wakati wa kupumua na baadaye kusababisha kutoka kwa sauti inayosikika ya kukoroma.

Kitendo hicho cha kuingia au kutoka kwa hewa huweza kuzuiwa na sababu mbalimbali ikiwemo hii ya kuziba tundu za pua kusiko kamili ambako husababisha nguvu zaidi kutumika katika kupitisha hewa kwenye pua wakati mtu akiwa amelala.


Miongoni mwa sababu zinazoweza kusababisha mtu kukoloma ni pamoja na kuwa na misuli dhaifu katika koo na ulimi. Suala hilo hutokea pale mtu anapolala fofofo! au kuwa na usingizi mzito na kusababisha kukoroma.


Hata hivyo, wanaume ndio hukabiliwa zaidi na tatizo hili kuliko wanawake hii ni kutokana na wanaume kuwa na njia nyembamba zaidi ya hewa kuliko wanawake, lakini tatizo hili pia huweza kusababishwa na kurithi. 


Pia tatizo hili huweza kusababisha madhara ambayo ni pamoja na kushindwa kulala vizuri yaani kuwa na usingizi wa mang’amung’amu, kutokana na hili mara nyingi watu hawa asubuhi huamka wakiwa wamechoka.

Kipimo cha tatizo hili mra nyingi ni lazima umshirikishe mwenzi wako au unayelala naye ili akuchunguze unapolala na kujua jinsi mwili wako unavyokuwa pale unapokoroma.


Unaweza kupunguza tatizo hili kawa kutokula mlo mkubwa kabla ya kulala, kutokunywa pombe kabla ya kulala pamoja na kutotumia vyakula au vinjwaji vyenye kafeini.


Vilevile wanaokoroma wanashauriwa kufanya mazoezi ya koo ambayo ni pamoja na kuimba na kusoma kwa kurudia rudia voweli (a,e,i,o,u) kwa nguvu kwa dakika kadhaa kwa siku.


Endapo unasumbuliwa na magonjwa sugu basi wasiliana na Mandai Herbal Clinic kwa simu namba, 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800, Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment