Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 3 September 2015

HIZI NDIZO FAIDA MUHIMU UTAKAZOZIPATA ENDAPO UTAANZA KUTUMIA ILIKI KAMA TIBA LEO

Iliki

ILIKI ni moja ya kiungo ambacho hutumika sana kwenye shughuli za mapishi ya jikoni husani katika kuandaa chai, licha ya kwamba ni kiungo tu lakini pia kina faida zake kwa afya.

Matumizi ya iliki husaidia sana kuipa uwezo mzuri figo wa kuondoa taka mwili ndani ya mwili, huku ikisaidia sana kuweka sawa mfumo wa umeng'enyaji chakula tumboni, kuondoa kiungulia, gesi tumboni pamoja na kuwasaidia wale wenye shida ya kukosa choo kwa muda mrefu.

Aidha, iliki imekuwa ikisifika sana kwa uwezo wake wa kusaidia kuweka sawa halufu ya kinywa, pamoja na kutibu shida ya vidonda vya mdomoni pamoja na matatizo yote ya kinywa na koo.

Pia iliki inauwezo mzuri sana wa kutibu matatizo ya maambukizi kwenye njia ya mkojo, matatizo ya figo na kibofu cha mkojo, sambamba na kupambana na magonjwa mbalimbali.

Iliki pia inauwezo wa kukabilina na hali ya mambukizi ya mafua sambamba na kikohozi pia 

Mbali na hayo, iliki pia inauwezo mzuri wa kukabiliana na matatizo ya saratani, pamoja na presha.

Kwa maelezo na ushauri zaidi fika Mandai Herbalist Clinic tupo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam au piga simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 barua pepe dkmandaitz@gmail.com


No comments:

Post a Comment