Sunday, 13 September 2015

HUU NDIO UKWELI WA SIFA ZA KARAFUU

 Habari za Jumapili mdau wa www.dkmandai.com leo napenda kukwambia hizi faida nyingine kuhusu karafuu.
 
Karafuu ni kiungo ambacho hupatikana sana hapa nchini hususani Zanzibar, huku kiungo hiki kikiweza kutumika peke yake au kwa kuchanganywa na viungo vingine.

Kiungo hiki kina sifa ya kuwa na ‘carbohydrates’ protini, mafuta (Volatile oil), nyuzi nyuzi ‘fiber’ ‘calcium,’ madini chuma na ‘potassium,’ pamoja na vitamin vitamin A na C.

Karafuu pia husaidia kuboresha uyeyushwaji wa chakula tumboni, huku ikisaidia pia kupunguza kichefuchefu, kutapika na kuharisha.

Sambamba na hayo, karafuu husaidia kulinda kuoza kwa meno na kufanya kinywa kuwa na harafu nzuri.

Unaweza kutumia kiungo hiki katika juisi ya matunda yenye uvuguvugu, supu, mchuzi au vinywaji vingine vilivyochemshwa.

Tafadhari endelea kuwa karibu nasi kwa kulike ukurasa wetu wa facebook uitwao Mandai Herbalist Clinic- mhc, ambapo utakuwa ukifikiwa na taarifa mbalimbali za tiba hususani tiba asilia, lakini pia kama unasumbuliwa na magonjwa sugu wasiliana na Dk Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.
 

No comments:

Post a Comment