Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 10 September 2015

HUU NDIO UMUHIMU WA KULA MATUNDA MARA KWA MARAKwa hali ya kawaida ni vziuri kuzingatia sana ulaji wa matunda kila siku, mara unapopata mlo wako .
Lakini kwa bahati mbaya si watu wote wamekuwa wakizingatia huu utaratibu wa kupendelea kula matunda kwa sababu mbalimbali wengine huenda ni kutokana na kuwa na kipato duni cha kumudu kupata matund ahayo, lakini wengine ni kutokana na kushindwa tu kutumia bila kuwa na sababu yoyote.

Tabia ya kutokula matunda husababisha mwili kukosa virutubisho muhimu ambavyo husaidia kujenga mwili na kuimarisha kinga za miili yetu.

Kwa kawaida miili yetu inapokosa kuwa na kinga imara husababisha mwili kushindwa kupambana dhidi ya magonjwa mbalimbali.

Mwili unapokuwa na kinga dhaifu, huwa ni rahisi sana kushambuliwa na magonjwa hatari ikiwemo saratani, ambayo kinga yake kubwa huwa katika upande wa ulaji wa matunda na mbogamboga.

Kufuatia kufahamu faida hizi chache kuhusu matunda naamini huenda kuanzia leo utaanza kuzingatia ulaji wa matunda kila unapopata nafasi hiyo.

Kwa ushauri zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0784 300 300, 0769 400 800, 0716 300 200 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment