Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 4 September 2015

HUU NDIO UWEZO WA ZABIBU TENA LEO


Zabibu hujulikana kama chanzo kizuri cha divai, lakini pia huweza kuliwa kama tunda na tunda hili hukuwa katika kichana chenye zabibu 6 hadi 300.  
Matunda haya huwa na rangi nyekundu iliyoiva, nyeusi, bluu ya kukoza , njano, kijani na hata pinki pia.
Mtaalam wa tiba asili Dk Abdallah Mandai anasema kwamba husaidia damu kuwa nyepesi na kuzuia isigande ndani ya mishipa ya damu, hivyo kutokana na sababu hii hupunguza hatari ya kukubwa na kiharusi (stroke)

Aidha, pia zabibu husaidia kuupa mwili nguvu na kuimarisha afya ya mishipa ya damu hususani ile inayosambaza damu kwenye nyama ya moyo. 

Pia tunda hili husaidia kuzuia na kutibu tatizo la upungufu wa damu na kwa wale wanaotumia mara kwa mara tunda hili huwasaidia kuepukana na ugonjwa wa bawasili pia.
Hali kadhalika, Dk Mandai anabainisha kuwa matunda hayo husaidia katika tiba na kinga ya magonjwa ya ini kutokana na uwezo wake wa kuliongezea ini uwezo wa kuondosha sumu mwilini na kuzalisha nyongo kwa wingi.

Zabibu pia husaidia kuimarisha afya ya figo na kuifanya kuwa na uwezo zaidi katika katika kuondosha sumu ndani ya damu .

Sambamba na hayo, juisi ya zabibu (divai) husaidia tumbo na utumbo kufanya kazi vizuri na kuzuia ukavu wa haja kubwa , lakini pia divai huimarisha afya ya mishipa ya damu katika mfumo wa kumeng;enya, kusaga na kusharabu chakula na viini lishe.

No comments:

Post a Comment