Friday, 11 September 2015

HUYU NDIYE MUFTI MPYA TANZANIA

Hatimaye Sheikh Abubakar Zubeir ametangazwa kuwa Mufti baada ya kushinda nafasi hiyo bila mpinzani jana, huku akiwataka Waislamu na Watanzania wengine kuhakikisha wanalinda amani na utulivu uliopo nchini.
Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi wa nafasi hiyo mjini Dodoma jana, Sheikh Zubeir aliwashukuru wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) kwa kumuamini na kuahidi kulitumikia baraza hilo na Waislamu wote kwa uadilifu mkubwa.
Alisema atahakikisha anatatua changamoto mbalimbali zilizopo ndani ya Bakwata na jamii ya Kiislamu nchini kwa kushirikiana na viongozi wenzake na kwamba atakuwa Mufti wa kuwatembelea Waislamu katika wilaya na mikoa yote na siyo kukaa ofisini.

No comments:

Post a Comment