Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 25 September 2015

IFAHAMU SEHEMU WANAPOISHI WATU WANENE KUPITA KIASI

Unene kupita kiasi ni moja ya matatizo ambayo yamekuwa yakiwazonga watu wengi kwa sasa, na watu wenye shida hiyo wamekuwa wakihangaika karibu kila siku katika kutafuta suluhisho la tatizo hilo.

Tatizo hili pia ni moja ya matatizo ambayo huwakabili baadhi ya Watanzania, lakini kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Afya Duniani (WHO) inaeleza kuwa watu wengi Ulaya ni wanene kupita kiasi.

Ripoti hiyo iliyopewa jina la European Health Report inasema asilimia 59% ya watu wanaoishi ulaya wana uzani uliozidi au ni wanene sana.

Shirika hilo limesema eneo la Ulaya lililochunguzwa, ambalo hujumuisha baadhi ya maeneo ya bara Asia, ndilo lililokuwa na viwango vya juu zaidi vya unywaji pombe na uvutaji sigara duniani.

Kutokana na hayo, maafisa wa WHO wameonya kuwa huenda vijana wa eneo hilo “wasiishi muda mrefu kama walivyoishi mababu zao”.

Mkurugenzi wa WHO anayesimamia Ulaya Zsuzsanna Jakab amesema: "Ripoti hii imeonyesha matumaini. Lakini bado kuna hatari iwapo uvutaji sigara na unywaji pombe utaendelea kwa viwango vya sasa. Hii inahusu sana vijana ambao huenda wasiishi muda mrefu kama mababu zao.”

No comments:

Post a Comment