Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 1 September 2015

ILE SHERIA YA MAKOSA YA KIMTANDAO NDIYO IMEANZA RASMI LEO, YAFAHAMU MAMBO YA KUEPUKA ILI UWE SALAMA


Jana Agosti 31, 2015 ndio ilikuwa siku ya mwisho ya yale mambo yote yanayokwenda kinyume na maadili kuonekana mtandaoni kwani sheria tayari imepitishwa na kuanza kutumika leo mahususi kwa wote wanaotumia vibaya mtandao.

Sheria hiyo imeanza kutumika rasmi baada ya kupitishwa na Bunge mapema 2015 na kusainiwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete ikiwa ni miongoni mwa sheria zilizopitishwa na bunge kwa hati ya dharura.

Hii ni sehemu ya orodha ya makosa ambayo yataweza kukufanya ushtakiwe

  • Kuweka mtandaoni picha za kingono za watoto
  • Kuweka mtandaoni picha za ngono au za utupu
  • Kuweka taarifa za uongo mtandaoni
  • Kuweka taarifa za uchochezi mtandaoni
  • Kutukana au kumdhalilisha mtu
  • Kuweka mtandaoni tetesi zisizothibitishwa
  • Kutukana au kumdhalilisha mtu kwa misingi ya udini/ukabila.
Innocent Mungi kutoka Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) anasema >>> ‘Ambaye atakua anachukua maamuzi ni jeshi la Polisi ambaye kwa mfano mtu akitukana kwenye mtandao au kufanya chochote kinyume na sheria yule aliyetendewa anao wajibu wa kulalamika kwa Polisi, watafanya uchunguzi alafu mwendesha mashtaka ataifikisha hiyo kesi kwa Jaji ambaye ndio atafanya maamuzi kutokana na kesi yenyewe‘

‘Sisi kama TCRA tunaweza kuitwa kama mashahidi kwenye hizo kesi, kwahiyo kuanzia August 31 2015 yale maswala ya mazoea ya NATUMA KAMA NILIVYOPOKEA au NINALETA KAMA NILIVYOIOKOTA HUKO, jihadhari sana kwa mfano yule aliyetengeneza amempelekea mtu mmoja lakini wewe umesambaza kwenye group lako la Whatsapp mko 100, utashtakiwa‘ – Innocent Mungi.


Source: Millard ayo.com

No comments:

Post a Comment