Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 3 September 2015

ISIKUPITE HII TAARIFA KUHUSU HALI YA HEWA.

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya kunyesha mvua nyingi za El–nino katika kipindi cha Oktoba hadi Desemba mwaka huu.

Kufuatia matarajio ya kuwepo kwa mvua hizo mamlaka zinazohusika zimetakiwa kuchukua tahadhari kwani kuna dalili za wazi za kunyesha mvua hizo ikiwemo kuongezeka kwa joto katika Bahari ya Pasifiki zaidi ya ilivyokuwa mwaka 1997 kuliponyesha mvua hizo.

Mkurugenzi wa mamlaka hiyo, Dk Agness Kijazi alisema hayo jana wakati akitoa utabiri wa mvua za vuli kwa kipindi hicho na kueleza kuwepo kwa mvua za juu ya wastani na wastani katika maeneo mengi yanayopata misimu miwili ya mvua na baadhi ya maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua.

Kijazi alisema suala la kunyesha mvua za El-nino linatokana na kuongezeka kwa joto katika Bahari ya Pasifiki pamoja na Bahari ya Hindi, lakini mpaka sasa joto la Bahari ya Pasifiki liko juu kufikia nyuzi joto 2.5 juu ya joto lililokuwa wakati wa mvua hizo mwaka 1997.

Alisema lakini joto la Bahari ya Hindi bado la wastani hivyo kuendelea kufuatilia mifumo ya hali ya hewa ili kuangalia iwapo joto hili litaongezeka kutakuwa na uhakika wa mvua hizo.

Dk Kijazi alisema kulingana na utabiri huo mvua zitaanza kunyesha kwa baadhi ya maeneo kuanzia wiki ya tatu ya mwezi huu hadi wiki ya nne ya Novemba na kumalizika Aprili mwakani.

Alisema katika maeneno machache ya kusini mwa nchi yatapata mvua chini ya wastani na mvua zitaanza mapema katika maeneo ya Kanda ya Ziwa Victoria na baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani kaskazini.

Akizungumzia baadhi ya maeneo, alisema ya ukanda wa pwani kaskazini katika maeneo ya Morogoro, Dar es Salaam, Tanga, Pwani na visiwa vya Unguja na Pemba, mvua inatarajia kuanza wiki ya mwisho ya mwezi huu na kuwa juu ya wastani na wastani.

Alisema kutokana na utabiri huo kuna hatari ya athari za unyevunyevu mkubwa wa udongo na kusababisha uharibifu wa mazao, ongezeko la magugu na magonjwa ya mimea pamoja na matumizi makubwa ya pembejeo hivyo kuongeza gharama za uzalishaji.

No comments:

Post a Comment