Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 9 September 2015

JE, UMEISIKIA HII TAARIFA YA MAMA ALIYEJIFUNGUA MTOTO MWENYE VICHWA VIWILI?

Mwanamke mmoja aliyekuwa mjamzito mkazi wa kijiji cha Chakonka Wilaya ya Uvinza, Kigoma amejifungua mtoto mwenye vichwa viwili na baada ya muda mfupi mtoto huyo alifariki.

Ilidaiwa kuwa mama huyo awali alikwenda kwenye kituo cha afya lakini hakupatiwa matibabu inavyotakiwa na hatimaye alikimbizwa kwenye hospitali ya rufaa ya Mkoa ambapo alijifungua kwa upasuaji.

Mume wake alisema mkewe alipata uchungu saa 8 usiku na kukimbizwa na usafiri wa boti usiku huo hadi kituo cha afya ingawa hawakuweza kumsaidia na baadaye alipelekwa Hospitali ya Rufaa Maweni.

Akithibitisha tukio hilo Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Shija Ganai alisema walimpokea mganga huyo saa 11 jioni na walipomchunguza walibaini mtoto ametanguliza miguu ndipo wakaamua kumfanyia upasuaji.

Anasema walibaini kuwa mtoto ana vichwa viwili ndiyo sababu ilichangia kufariki dunia mapema kutokana na kubanwa.

No comments:

Post a Comment