Wednesday, 16 September 2015

JE, UNAFAHAMU FAIDA ZA MADINI YA 'ZINC' MWILINI? ZOTE ZIPO HAPA NA VYANZO VYA MADINI HAYO PIA


Habari za leo mdau wa www.dkmandai.co sina shaka utakuwa umzima, lakini kama ni tofauti na hivyo apenda kukupa pole sana.

Leo napenda kuanza kwa kuuliza hili swali, ingawaje sitahiyaji majibu na badala yake utakuwa ukijijibu mwenyewe moyoni, swali lenyewe ni hili hapa "Hivi ni mara ngapi umekuwa ukisikia kuhusu faida za madini ya zinc mwilini mwako? na je, unaposikia kuhusu madini haya ya zinc huwa unaelewa nini?

Maswali hayo mawili hapo juu naomba nitayajibu kama ifuatavyo hapa chini kwani kuna watu wengi wameniuliza maswali hayo kwa njia ya sms kupitia namba ya Mandai Herbalist Clinic ya 0769 400 800.

Kwanza kabisa madini haya ya 'zinc' yana nafasi kubwa na umuhimu sana katika kuimarisha kinga zetu za mwili na hivyo kutufanya kuwa ni vigumu kukubwa na magonjwa mbalimbali.

Pale mtu unapokuwa na kiwango kidogo cha madini ya 'zinc' basi mhusika huwa anakuwa katika nafasi kubwa ya kuwa na kinga ambazo si imara hivyo kusababisha urais wa mhusika kukubwa na magonjwa.

Pia mtu mwenye madini ya zinc hafifu hukosa hamu ya kula, huwa na nywele zisizokuwa na afya pamoja na kuwa na ngozi mbaya.

Unaweza kuyapata madini haya ya zinc kupitia mbegu za tunda la tikiti maji, mbegu za tunda hilo zina asilimia 70% ya kiwango cha madini ya 'zinc'.

Ulaji wa maboga pia ni chanzo kimojawapo kizuri cha madini ya zinc, hivyo unaweza kutumia pia maboga kama chanzo cha madini haya.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi Mandai Herbalist Clinic kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com


No comments:

Post a Comment