Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 21 September 2015

KENYATTA ASISITIZA KUTOWALIPA WALIMU ASEMA NCHI HAINA UWEZO WA KULIPA NYONGEZA YA MISHAHARA

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya
Wakati shule zote za umma na binafsi zikianza kufungwa kuanzia hii leo nchini Kenya Rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta amesisitiza kwamba serikali yake haina uwezo wa kulipa nyongeza ya mishahara wanayodai walimu wanaoendelea na mgomo.
Hayo aliyasema alipokuwa akihutubia taifa hilo kwa njia ya televisheni, huku akitoa wito mgogoro huo kutatuliwa kwa amani na kusema kuwa shule zote zinafungwa kuanzia leo.

Serikali ya Kenya imeagiza shule zote nchini humo zifungwe kuanzia leo huku mgomo wa walimu ukiendelea.

Barua kutoka kwa wizara ya elimu imeagiza shule zote za umma na za kibinafsi zifungwe na wanafunzi warudi nyumbani, huku watakaosalia shuleni pekee ni wanafunzi wanaojiandaa kufanya mitihani ya kitaifa ya darasa la nane na kidato cha nne mwaka huu.

Katibu Mkuu wa chama cha walimu nchini humo KNUT ameiambia BBC kuwa tayari amepokea barua hiyo ya kufungwa kwa shule kutoka kwa serikali.

Amesema chama hicho kilikuwa kimeishauri serikali ifunge shule "zamani". Mahakama inatarajiwa kuamua Ijumaa ijayo iwapo mgomo huo wa walimu, ambao umelemaza masomo muhula wa tatu, ni halali au la.


CHANZO : BBC SWAHILI

No comments:

Post a Comment