Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 21 September 2015

KULA VYAKULA HIVI ILI KUIMARISHA AFYA YA NGOZI YAKO BILA KUHANGAIKA NA VIPODOZI


Bila shaka kila mtu anatamani kula chakula chenye virutubisho sahihi kila siku ili kuwa na afya njema.


Hapa duniani kuna vyakula vya asili ambavyo ndani yake kuna virutubisho muhimu vinavyosaidia mwili kupambana na magonjwa na pia kuimarisha afya.


Vyakula hivyo si vingine bali ni vile vya kijani ambavyo vina uwezo mkubwa zaidi katika kuponya magonjwa na kusaidia pia kurekebisha na kujenga mwili na kuimarisha siha.


Ngozi ni moja ya sehemu muhimu ya mwili ambayo ina jukumu kubwa la kuukinga na kuufunika mwili na viungo mbalimbali na afya yake ni jambo la kuzingatiwa.


Vifuatavyo ni vyakula vinavyoweza kusaidia kuimarisha afya ya ngozi:-

Chakula cha kwanza chenye uwezo wa kuimarisha siha ya ngozi ni asali. Asali husaidia kutunza na kuhifadhi unyevu kwenye ngozi na ina kiwango kikubwa cha sukari paka asali wakati wa kuoga, acha kwa muda kisha ioshe. Kufanya hivyo kunaweza kuinawirisha ngozi.


Aidha, vyakula vya baharini kwa ujumla wake huwa ni vizuri kwa afya, lakini faida haishii kwenye afya ya mwili tu, bali inasaidia hata kwenye ngozi. Vyakula vingi vya baharini vina kiwango kikubwa cha Zinc na Omega 3 ambazo ni muhimu kwa siha ya ngozi. Faida za Omega 3 ni pamoja na kuondoa kukakamaa au ukavu wa ngozi, kupunguza kuvimba na kukunjamana kwa ngozi na husaidia mzunguko mzuri wa damu mwilini hivyo kuboresha afya ya ngozi. Damu inapozunguka vyema mwilini afya ya ngozi hayo huimarika.


Nisikuchoshe kusoma sana mdau wangu wa www.dkmandai.com hayo ndiyo machache yatakayokusaidia kuimarisha ngozi, lakini kwa mengine mengi wasiliana nasi Mandai Herbalist Clinic kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment