Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 22 September 2015

KWELI CCM MBELE KWA MBELE UTAFITI WAFANYWA MATOKEO YAONESHA INAONGOZA KWA 66% UKAWA WAGALAGAZWA

Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) na upande wa kulia ni mgombea urais kwa tiketi ya CCM  Dk. John Magufuli (picha kwa msaada wa mtandao)
Ikiwa zimesalia siku 32 kufikia Oktoba 25 siku ambayo uchaguzi Mkuu utakwenda kufanyika na Watanzania watafanya maamuzi yao ya kuwachagua viongozi wanaowapenda mara baada ya kusikiliza sera zao na kuzitathimini kwa makini

Sasa wakati hayo yakiendelea na Watanzania wakiisubiri siku hiyo ya uchaguzi kwa hamu, Taasisi ya Twaweza imetoa utafiti wake ambao inasema imefanya kwa wananchi wa Tanzania bara  kutoka mikoa tofauti ya Tanzania,.

Utafiti huu ulikuwa ukiuliza swali la kama uchaguzi ungefanyika leo, ungempigia kura mgombea wa chama gani? Kwa mujibu wa utafiti huo wanasema watu walijibu kama ifuatavyo.

·         CCM - 66%
·         CHADEMA – 22%
·         CUF – 1%
·         ACT WAZALENDO- 0%
·         UKAWA – 3%
·         KINGINE- 6%

·         HAKUNA JIBU -2%
No comments:

Post a Comment