Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 10 September 2015

KWELI HAPA KAZI TU..!! SOMA HAPA HIZI SIFA ZA MAWAZIRI ANAZOZITAKA DK. MAGUFULI ENDAPO AKIWA RAIS

Ikiwa bado mchakamchaka wa kampeni ukiendelea nchini, huku wagombea wakipita huku na kule kunadi sera zao na kuonesha dhamira zao za dhati za kuwatumikia Watanzania, mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli yeye ameamua kuweka wazi sifa za watu atakaowajumuisha katika baraza lake la mawaziri pindi atakapochaguliwa kuwa rais.

Akizungumza mbele ya umati katika mkutano wake wa kampeni jana, Magufuli alisema sifa mojawapo kubwa ya mtu atakayemteua katika baraza lake la mawaziri ni kutokuwa bingwa wa kutoa visingizio vya hapa na pale katika kuhalalisha ucheleweshaji wa huduma kwa wananchi.
 

Magufuli alisema sifa ya pili ya mtu atakayemteua kushika nafasi ya uwaziri katika serikali yake ni kuchapa kazi bila kuchoka katika kushughulikia matatizo ya wananchi, huku akigusia kauli mbiu yake ya “Hapa Kazi Tu”.

Kuhusu sifa ya tatu Magufuli alisema waziri atakayemteua atatakiwa kuwa ni anayejali matatizo ya wananchi na hata mvumilia ambaye atatelekeza ofisi na kwenda kwenye shughuli zake binafsi.  


Sifa ya nne kwa waziri atayekuwamo katika serikali yake ni kujali muda katika kushughulikia kero za wananchi; kwamba kila tatizo likifikishwa kwake alishughulikie kwa wakati na si kinyume chake.

“Nitaweka aina ya mawaziri ambao wao ni kazi tu… wakipelekewa matatizo ya wananchi wanayatatua kwa wakati na sitaki kusikia visingizio kama mchakato unaendelea wala nini… nataka kazi tu,” alisema Dk. Magufuli na kusababisha shangwe kubwa kutoka kwa wananchi waliofika kwa wingi kumsikiliza.

Katika sifa ya tano, Magufuli alisema kila waziri atakayemteua ni lazima aonyeshe wazi kuwa anayo dhamira ya dhati ya kuwatumikia Watanzania na mara zote atafanya kazi kwa kujua kuwa kipaumbele kikubwa ni kuwatumikia wananchi waliowachagua.

Magufuli alitaja sifa ya sita muhimu zaidi kwa mawaziri wake ni uadilifu na wasiotiliwa shaka na wananchi watakaokuwa wakiwatumikia, huku wakijua kuwa wengi wao (wananchi) ni watu maskini wanaohitaji huduma zote muhimu za kijamii ili kujikwamua kiuchumi.

Mbali na hayo Magufuli alisema kuwa “Nikiwa Rais nitakuwa mtumishi wa Watanzania wote. Uwe CUF wewe ni wangu, ACT – Wazalendo, Chadema, NCCR – Mageuzi wote nitakuwa mtumishi wenu. Hivyo naombeni kura zenu niweze kuwatumikia katika kuleta maendeleo.,” 

Tangazo: Kama unasumbuliwa na magonjwa sugu wasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment