Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 25 September 2015

LEO NI NAFASI YA KUYAFAHAMU HAYA MENGINE KUHUSU FAIDA ZA ALO VERA KATIKA TIBA

Alo vera ni mmea unaopatikana porini na unafanana sana na mmea wa katani na una miiba pembeni, lakini kuna aina nyingi ya mmea huu isipokuwa hapa nataka kuzungumzia ile alovera ambayo ni chungu. 

Mmea huu unasifika kwa kuwa tiba ya maradhi mbalimbali pamoja na uchungu wake, miongoni mwa magonjwa hayo ni pamoja na malaria, kuumwa na wadudu, baridi yabisi.

Mtaalam wa tiba asili kutoka Mandai Herbalist Clinic, Tabibu Abdallah Mandai anasema kwamba alo vera pia huleta hamu ya kula na husaidia mmeng'enyo wa chakula tumboni sambamba na kuwasaidia wale wenye matatizo ya shida ya haja ndogo (mkojo) kutoka kwa shida.

Aidha magonjwa mengine ambayo huweza kutibika kwa kutumia alo vera ni pamoja na shinikizo la damu la juu, saratani (cancer) bawasira, mkanda wa jeshi na kusaidia askari wa kulinda mwili.

Pamoja na hayo, Tabibu Mandai anabainisha kuwa alo vera nayo husaidia kuongeza nguvu za kiume na kuwasaidia wale wenye shida ya kuvimba mwilini.


Angalizo: Dawa hii ya alo vera hatakiwi kabisa kutumia mama mjamzito au anayenyonyesha usijaribu kutumia kama upo katika hali hizo tafadhari. 

Asante sana kwa kusoma hizi faida za alo vera na hizo ni baadhi ya faida zinazotokana na alo vera katika masuala ya tiba, lakini kama unasumbuliwa na magonjwa sugu ni vyema ukafanya utaratibu wa kufika Mandai Herbalist Clinic, kituo kilichopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na utapata tiba ya magonjwa yako au wasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment