Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 24 September 2015

LEO NINAZO HIZI SIFA ZA UBUYU KATIKA TIBA

Mbuyu ni kati ya miti mikubwa na minene inayopatikana katika ukanda wa tropiki, Matunda yake yanaitwa mabuyu, gamba la tunda hilo huitwa kibuyu na ubuyu ni nyama ya tunda.

Mti huu umesheheni malighafi nyingi na nzuri katika afya ya binadamu, ambapo inaelezwa unga wa ubuyu huwa na vitamin na madini mengi, kwani unga huo una kiasi cha vitamin C nyingi kushinda ile inayopatikana kwenye chungwa.

Aidha, Tabibu Abdallah Mandai kutoka Mandai Herbalist Clinic anabainisha kuwa mti huo wa mmbuyu husaidia kutibu homa, ambapo mgonjwa atapaswa kuchemsha magome yam mea huo.

Mtaalam huyo anaendelea kueleza kwamba mti huo unauwezo wa kutibu ugonjwa wa malaria, kifua kikuu pamoja na pumu pale magome yake yanapotumika mara baada ya kuchemshwa.


Pamoja na hayo, Tabibu Mandai anafafanua kuwa kwa wale wenye shida ya kikohozi wanapaswa kuchanganya unga wa tunda lake pamoja na asali kisha mgonjwa atalamba au kutumia kwa kuchanganja na maji ya moto.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment