Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 19 September 2015

MANENO YA WAZIRI SIMBACHAWENE KUHUSU KUANZA KWA MATUMIZI YA UMEME WA GESI

.
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene September 18 2015 alionge na waandishi wa habari kuhusu mradi wa bomba la gesi na kuwashwa kwa mitambo ya kuzalisha umeme ya Ubungo na Kinyerezi.

Akizungumza kuhusu hayo Simbachawene alisema ‘‘Mtakumbuka kwamba mwaka 2012 serikali ilianza mchakato wa kutekeleza mradi mkubwa wa bomba la gesi ambalo kukamilika kwake kungesaidia sana kuondoa matatizo ya umeme nchini.


Akifafanua zaidi Simbachawene alisema kazi hiyo ilijumuisha ujenzi wa mtambo wa kuchakata gesi wa madimba (Madimba Processing Plant), mtambo wa kuchakata gesi wa Songosongo (SongoSongo Processing Plant) na Bomba kubwa la kusafirisha gesi kutoka Mtwara na kuja Dar es Salaam

Hata hivyo, waziri huyo alisema mitambo iliyoanza kuzalisha umeme ni ya Megawati 90 tu kwa sasa, huku akisema kwamba wanaendelea kufuatilia ufanisi wa bomba na hasa msukumo wa gesi pamoja na vigezo vingine vya kitaalamu kabla yakuwasha mitambo mingine kutokana na mfumo wote wa bomba ni mpya hivyo inawalazimu kuiingiza kwa uangalifu ili kuepusha madhara katika mfumo wa bomba.

Katika hatua nyingine waziri huyo alisema "kila mtambo una kiwango chake cha msukumo wa Gesi kinachoruhusu mtambo husika kuwaka, hivyo kwa kadri viwango vya msukumo wa Gesi katika Bomba vinavyozidi kuimarika ndivyo uzalishaji wa umeme utakavyoendelea kuongezeka.Hii ina maana kwamba upungufu wa umeme uliokuwepo utaendelea kupungua hatua kwa hatua kulingana na mitambo hii inavyoendelea kuwashwa na kuzalisha umeme"

No comments:

Post a Comment