Saturday, 26 September 2015

OGOPA KUTOA MIMBA MADHARA YAKE NI MAKUBWA NI BORA UKASUBIRI UJIFUNGUE TU! SOMA HAPA MADHARA YAKE
Habari za weekend mdau wangu wa www.dkmandai.com naamini kwamba utakuwa mzima kwa siku hii ya leo.

Kwa sasa naomba niweze kujibu swali la mdau wa tovuti hii aliyeuliza kupitia namba yetu ya 0769 400 800 ambapo yeye alihitaji kujue endapo kutoa mimba kuna madahara yoyote.

Hivyo napenda kujibu swali hili kwa faida yake pamoja na wadau wengine wa tovuti hii kama ifuatavyo:

Kwanza kabisa ifahamike kwamba kitendo cha kutoa mimba katika nchi yetu ni kosa la kisheria,

Lakini pia kitendo hicho huweza kuwa namadhara kwa sababu wengi wanaotoa mimba hawatoi mimba chini ya uangalizi wa kitaalamu hivyo kusababisha zoezi hilo kuharibiwa kuta za mji wa mimba.

Pia mbali na kusababisha uharibufu wa kuta hizo, lakini pia huchangia maambukizi kwenye mji wa mimba na pia kuharibu mfumo wa mji wa mimba.

Endapo madhara haya yatajitokeza basi inawezekana mtu kukosa mtoto kwa sababu ya kuharibu kizazi.

Mbali na hayo ni vyema ikafahamika pia kitendo cha kutoa mimba pia ni moja ya vitendo vibaya ambavyo vinapigwa vita na dini zote hapa duniani.

No comments:

Post a Comment