Tuesday, 22 September 2015

PALE UNAPOKUMBWA NA MAUMIVU MAKALI YA SIKIO, TUMIA KIUNGO HIKI UTAPONA


Hivi ushawahi kuumwa sikio? ikiwa kama bado hujawahi kukubwa na maumivu ya sikio basi nikupe hongera yako na ni vyema ukaomba Mungu usikumbwe na maumivu ya sikio.

Dhamira yangu si kukwambia au kukusimulia kuhusu uchungu wa maumivu ya sikio, lakini nilipenda utambue kwamba maumivu ya sikio ni kiboko hivyo unapopatwa na hali hiyo usije kudharau kabisa.

Si ajabu kabisa mtu mwenye maumivu ya masikio kukosa usingizi, au kupatwa na maumivu makali ya kichwa na wakati mwingine hupelekea homa kabisa, huku sikio likiambatana na milio au kelele za ajabu ajabu muda wote.

Sasa napenda kukufahamisha wewe mdau wangu hizi mbinu za kujitibu mara utakapokumbwa na maumivu ya sikio kama ifuatavyo:

Kwanza unaweza kutumia kitunguu maji ili kusaidia kutuliza maumivu ya sikio, unachopaswa kufanya ni kudondosha matone mawili ya jusi ya kitunguu maji ndani ya sikio lenye maumivu kisha kaa kwa dakika kama moja hivi au mbili kisha geuza kichwa ili kuiruhusu juisi ya kitunguu uliyoweka itoke ndani ya sikio lako, Fanya tiba hii mara mbili kwa siku asubuhi na jioni.

Kama utaona huweza kutumia juisi hiyo ya kitunguu maji basi unaweza kutumia juisi ya majani ya muembe, hii nayo utapaswa kuitumia kwa kuweka kwenye sikio lililo na tatizo. Lakini kama utahitaji kujua jinsi ya kuandaa juisi hii ya majani ya muembe ili ikusaidie kwa tatizo hilo basi unaweza kumpigia Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment