Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 28 September 2015

PATA NAFASI YA KUYAFAHAMU MENGINE YA MUHIMU KUHUSU ZABIBUZabibu ni matunda matamu yanayopendwa, huku yakiwa na faida nyingi kiafya, hapa nchini matunda haya hupatikana zaidi Dododma.

Zabibu ambazo wengi wentu tumezoea kuziona na ambazo tunazifahamu pia ni zile zabibu za rangi nyeusi, lakini kuna zabibu za rangi ya kijani na nyekundu pia.

Matunda ya zabibu ndiyo matunda pekee ambayo hutumika kutengenezea mvinyo 'wine' sehemu mbalimbali duniani.

Miongoni mwa faida za zabibu kiafya ni pamoja na kusaidia kuweka sawa mmeng'enyo wa chakula na hivyo kusaidia kuondoa tatizo la kukosa choo.


Aina za Zabibu
Zabibu husaidia kuongeza unyevunyevu kwenye njia ya hewa na hivyo kupunguza utokeaji wa pumu.

Ndani ya zabibu kuna madini ya chuma na manganizi, madini haya ni sehemu ya kujenga mifupa imara na kusaidia sana kuongeza damu mwilini kutokana na kuwa na madini chuma.

Zabibu pia husaidia sana kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo pamoja na saratani na kusaidia kuzuia mafuta kulundikana kwenye mishipa ya damu.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment