Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 28 September 2015

R.I.P CELINA KOMBANI, NI VILIO NA SIMANZI VIMETAWALA KATIKA ZOEZI LA KUAGA MWILI WAKE DAR ES SALAAM LEO (PICHA ZOTE ZIPO HAPA)

Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais  (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), Celina Kombani umeagwa leo jiji Dar es Salaam katika viwanja vya Karimjee kabla ya kusafirishwa kuelekea nyumbani kwake Mkoani Morogoro kwa ajili ya maziko yatakayofanyika kesho shambani kwake.

Zoezi hilo la kuaga mwili wa marehemu limeongozwa na Makamu wa Rais, Dk Gharib Bilali pamoja na Mama Salma Kikwete na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na ndugu jamaa na Watanzania kwa ujumla.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo Spika wa Bunge Mama Anne Makinda amesema kuwa marehemu alikuwa ni mchapakazi, muadilifu na mchezi pia, na ameacha pengo kwa familia yake pamoja na serikali kwa ujumla.

Makinda pia amewataka Watanzania kuchukulia kifo hicho kama somo na kujifunza kuishi kwa upendo kwani hakuna anayeijua kesho yake.

Ninazo picha hapa za zoezi zima la kuaga mwili wa marehemu Celina Kombani.No comments:

Post a Comment