Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 1 September 2015

SASA NI ZAMU YA JUISI YA LIMAO NA FAIDA ZAKE ZOTE NIMEKUWEKEA HAPA, KARIBULimao ni moja ya tunda ambalo linafahamika sana, ni tunda ambalo mara nyingi hutumika zaidi jikoni kwa ajili ya kukata shombo fulani fulani ya baadhi ya mboga mfano samaki.

Kwa kawaida limao huwa na ladha ya uchachu, lakini pamoja na kuwa na ladha hiyo tunda hili limekuwa na faida pia za kiafya.

Limao linasifika sana kwa kuwa  vitamin C, B protini na carbohydrates, lakini pia kuna anti-oxidant ambayo husaidia kupambana na saratani.

Juisi ya limao inafahamika pia kwa kuwa na uwezo wa kukabiliana na matatizo ya mawe kwenye figo, kupunguza hatariya kupata kiharusi 'stroke' pamoja na kushusha joto la mwili.

Aidha, juisi ya limao pia ni kinga nzuri ya matatizo ya usagaji wa chakula pamoja na ukosefu wa choo 'constipation' inaaminika kuwa kiasi cha matone kadhaa ya limao katika kinywaji chako huwa ni msaada mkubwa wa matatizo hayo ya umenge'nyaji wa chakula na ukosefu wa choo, lakini pia unapokunywa juisi ya limao mara baada ya chakula chako cha mchana au usiku husaidia kurahisisha mzunguko mzuri wa damu ndani ya mwili.

Pia juisi ya limao ni kinga nzuri ya magonjwa ya kinywa na meno, kwani juisi hiyo huwasaidia wale wenye shida ya kutokwa na damu kwenye fizi, lakini pia huondoa tatizo la harufu mbaya kinywani na husaidia kung'arisha meno.

Kwa wale wenye shida ya mba za kwenye nywele, basi nao wanaweza kutumia limao ili kuondokana na shida hiyo, pia unapotumia juisi ya limao husaidia kukuza nywele na kuzifanya kuonekana zinang'aa na asili zaidi.

Kuhusu urembo pia limao husaidia sana kuondoa mikunjo ya uso 'wrinkles' kinachofanyika katika urembo huu ni kupata juisi ya limao iliyochanganya na maji kiasi pamoja na asali.

Mbali na hayo, juisi ya limao pia husaidia kupunguza uzito hasa kwa wale wenye uzito mkubwa, lakini pia husaidia sana kukabiliana na shida ya magonjwa ya upumuaji hususani pumu hasa mhusika anapokuwa anatumia juisi hiyo mara kwa mara.

Angalizo si vyama kutumia limao nyingi sana kwani huweza kukupelekea kwennye tatizo la anemia.

Kama utakuwa na swali, maoini au ushauri unaweza kuwasiliana na Tabibu wako Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkamandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment