Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 24 September 2015

SIKUKUU ZINA MAMBO MENGI HEBU JARIBU KUEPUKA UNYWAJI WA POMBE SIKUKUU HII MADHARA YAKE NI MAKUBWALeo Septemba 24, 2015 ni Idd El Hajj hii ni sikukuu kwa waumini wa dini ya kiislam, lakini watu wengi kwenye sikukuu kama hizi huzitumia vibaya kwa kufanya starehe na kunywa vileo mbalimbali.

Sasa hapa nakukutanisha na Tabibu Abdallaha Mandai kutoka Mandi Herbalist Clinici ambaye ameamua kuelezea madhara ya unywaji wa pombe.

Tabibu Abdallah Mandai anasema kuwa, kiafya matumizi ya pombe huleta madhara mbalimbali ndani ya mwili wa binadam, kwa mfano ini huathirika vibaya kutokana na matumizi ya pombe kupindukia, lakini pia tumbo nalo huathirika kutokana na kuchubuka kwa ngozi laini ya tumbo la chakula na kusababisha vidonda vya tumbo.

Tabibu Mandai anaeleza kuwa, pia pombe huleta madhara katika moyo na mapafu ya binadamu, lakini pia kwa upande wa wanawake wajawazito pombe huwasababishia kuharibika kwa mimba na hata kupelekea kujifungua mtoto mwenye mtindio wa ubongo.

Tabibu Mandai anafafanua kuwa pombe imekuwa na madhara mengi yakiwemo yale ya moja kwa moja na yanayokuja taratibu, ambapo mtaalam huyo anaeleza kuwa pombe husababisha mtu kutetemeka, kuzubaa zubaa na hata kupauka kwa mwili.

Mtaalam huyo anaeleza kwamba, pombe pia huleta madhara kama vile upungufu wa nguvu za kiume, kukosa hamu ya tendo la ndoa (loss of libido), saratani ya figo na kufanya figo kushindwa kufanya kazi yaani (renal failure).

Licha ya madhara hayo pia pombe husababisha saratani ya ini, kusinyaa kwa ini na hata saratani ya tumbo sambamba kabisa na vidonda vya tumbo.

Hata hivyo, Tabibu Mandai anasema, mbali na madhara ya kiafya, pia pombe huleta mifarakano ndani ya jamii na hata kuvuruga na kuondoa amani ndani ya familia, huku ikiathiri uchumi wa mtu kwani pombe ikishakuwa sugu ndani ya mwili wa binadamu (chronic), watu wengi huishia kumaliza vipato vyao kwa ajili ya kununua kinywaji hicho.
Tabibu Mandai anasema pamoja na kuwepo kwa tahadhali katika matangazo ya pombe lakini bado kinywaji hicho kimekuwa na wanywaji wengi, hivyo anasema ni vizuri ukahakikisha unaepuka matumizi ya pombe kupindukia kwa ajili ya kulinda afya yako.

Kwa ushauri wasiliana na Tabibu Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment