Friday, 11 September 2015

TABIBU MANDAI ANAKUFAHAMISHA HIZI SABABU ZA KUHISI MAUMIVU WAKATI WA TENDO LA NDOA

Tabibu Abdallaha Mandai ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Mandai Herbalist Clinic
Maumivu wakati wa kushiriki tendo la ndoa ni moja ya tatizo ambalo huwakabili baadhi ya watu na kusababisha baadhi yao kulichukie kabisa tendo hilo na hata kukosa hamu ya kushiriki kabisa.

Akielezea tatizo hilo Tabibu Abdallah Mandai kutoka Mandai Herbalist Clinic, anasema, mara nyingi maumivu ambayo hujitokeza mwanzoni wakati wa tendo la ndoa halafu yanapotea baadaye, hali hii husababishwa na upungufu wa ute unaoilainisha njia ya uzazi (uke) na mara nyingi hutokana na maandalizi hafifu wakati wa tendo husika.


Aidha, Tabibu Mandai anasema mbali ya sababu hiyo pia tatizo hili wakati mwingine hutokea baada ya mwanamke kumeza dawa zinazohusisha majimaji ukeni kama vile dawa za kuzuia uzio na nyinginezo. japo si mara zote huweza kuleta hali hiyo.


Pia Tabibu Mandai anaeleza kuwa, tatizo hilo huweza kusababishwa na athari za kisaikolojia anazokuwa nazo mwanamke. Mfano, kama mwanamke aliwahi kubakwa au kufanyiwa vitendo viovu mara nyingi mwanamke wa aina hiyo huweza kuwa na hali ya kutohisi hamu ya tendo la ndoa na badala yake akishiriki tu basi hujikuta akiambulia maumivu.


Tabibu Mandai anaendelea kusema kwamba, tatizo hili huweza kuwapata wanawake ambao muda wao wa kupata hedhi umekoma 'menopause' , hii ni kwa sababu baadhi ya vichocheo (homoni) vinavyochochea kutolewa kwa majimaji ili kulainisha njia ya uzazi hupungua kwenye damu, huku wengine wakiwa ni wale wenye matatizo ya maambukizi ya magonjwa katika viungo vyao vya uzazi hususani magonjwa ya zinaa.

Pia maambukizi kwenye njia ya mkojo hasa kwenye kibofu cha mkojo huleta maumivu wakati wa tendo la ndoa, hali kadhalika na wale wanawake wenye matatizo sugu ya kukosa choo wao nao wanauwezekano mkubwa wa kupata maumivu haya.


Mbali na sababu hizo pia endapo mwanamke atafanya tendo la ndoa kipindi kifupi mara baada ya kujifungua huweza kupata maumivu wakati wa tendo hilo. Hii ni kwasababu mwanamke anapojifungua, viungo vyake vya uzazi huchukua muda mrefu hadi kurudi katika hali yake ya kawaida, hivyo basi anaposhiriki tendo la ndoa muda mfupi baada ya kujifungua kunakuwa na uwezekano mkubwa wa kuhisi maumivu. Pia tatizo hili huwapata wanawake waliojifungua kwa kuongezwa njia ya uzazi.

Kama unaushauri, swali au maoni unaweza kuwasiliana na Tabibu Mandai sasa kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment