Sunday, 6 September 2015

TABIBU MANDAI HAPA ANAKUELEZA SABABU ZINAZOPELEKEA MTU KUPATA KIHARUSI 'STROKE' SOMA ILI UJIKINGE

Ugonjwa wa kiharusi 'stroke' ni moja ya magonjwa yasiyoambukizwa, ambao husababisha hali ya mwili kupooza kutokana na matatizo ya mishipa ya damu inayolisha ubongo.

Matatizo hayo ya mishipa ya damu huweza kuwa ni kutokana na kuziba au kupasuka kwa mishipa hiyo ya damu, hivyo kuchangia seli za ubongo kufa haraka kutokana na kukosa oksijeni ya kutosha na lishe ya kawaida ambavyo vyote hivyo huhitajika kufika kwenye ubongo kwa njia ya mishipa hiyo ya damu.
Muonekano wa mtu aliyepata kiharusi
Aidha, ni vyema ikafahamika kuwa kiharusi 'stroke' ni hali ya dharura inayoweza kutibiwa endapo tatizo litafahamika na kutibiwa kwa haraka, lakini lisipotibika husababisha mhusika kupooza katika hali mbalimbali.

Hayo ni maelezo machache tu kuhusu ugonjwa wa kiharusi, lakini kama utapenda kufahamu namna ya kukabiliana na ugonjwa huo kwa kutumia tiba asili ni vyema ukatazama kipindi cha Mandai Afya. com leo Jumapili Septemba 06, 2015 kupitia STAR TV kuanzia saa 1: 25 hadi saa 2:00 USIKU, ambapo Tabibu Abdalaha Mandai ataeleza namna ya kutibu ugonjwa huo kwa njia asili. Usikose ili ujifunze zaidi namna ya kuondokana na tatizo hilo.

Pia unaweza kuwasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kwa namba za simu zifuatazo; 0716 300 200,  0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment