Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 25 September 2015

TABIBU MANDAI LEO ANAKUFAHAMISHA MAAJABU YA MZAMBARAU KATIKA TIBA, KUMBE NI NZURI KWA MATATIZO YA KINAMAMA NA KINABABA


Kila siku ya Ijumaa Tabibu Abdallaha Mandai huwa anazungumza kuhusu tiba za mimea kuanzia saa 5:30 hadi 6:00 mchana kupitia Redio Times (100.5) ndani ya kipindi cha 'Hatua 3' na leo Septemba 25 alifanya hivyo pia.

Sasa huenda wewe hukuweza kusikiliza alichokizungumza siku ya leo kupitia kipindi hicho basi usipate tabu nimekukusanyia dondoo zote muhimu alizozungumza leo.

Kwanza kabisa ni vyema ifahamike kuwa alizungumza kuhusu faida za Mzambarau na yafuatayo ni matatzi ambayo huweza kutibika kwa kutumia mti huo.

Tabibu Mandai alisema kuwa mti wa mzambarau huweza kutumika kama tiba kuanzia mizizi yake, majani na magome pia.

Kuhusu mizizi ya mzambarau Tabibu Mandai anasema ukiichimba na kuchemsha kisha ukatumia kwa kunywa glasi moja asubuhi na jioni kila siku hiyo huweza kuwa njia nzuri ya kuwasaidia kinamama wenye shida ya kupata siku zao, licha ya kwamba hawajafikia muda wa kufunga hedhi yaani 'menopause'

Magome ya mzambarau Tabibu Mandai anasema husaidia sana kuimarisha kinga za mwili na kuwasaidia kinababa wenye shida ya nguvu za kiume, kinachofanyika ni kupata magome na kuyakausha kisha kuyasaga halafu utatumia unga huo wa magome kwa kupima kijiko cha mezani ndani ya maji ya uvuguvugu au uji kila siku asubuhi na jioni na itakusaidia sana.

Pia unga huo wa magome nao huweza kuwasaidia wenye tatizo la kisukari kwani husaidia sana kusawazisha kiwango cha sukari mwilini, lakini si kutibu kisukari bali kuweka sawa kiwango cha sukari mwilini.

Hata hivyo Tabibu Mandai alieleza pia kuhusu ugonjwa wa bawasiri au mgolo (kuuta kinyama sehemu ya haja kubwa) ambao nao unaweza kutibika kwa kutumia majani ya mzambarau kinachofanyika ni kuchemsha majani ya mzambarau na utayaacha yapoe kisha utatumia maji hayo kwa kunawa sehemu ya haja kubwa.

Lakini kwa maelezo zaidi unaweza kumtafuta Tabibu Abdallaha Mandai ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Mandai Herbalist Clinic kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800


No comments:

Post a Comment