Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 2 September 2015

TANESCO YAKANUSHA KUHUJUMU KAMPENI ZA BAADHI YA VYAMA KWA KUKATA UMEME

Hivi karibuni kumekuwa na hali ya kukatika kwa umeme mara kwa mara katika maeneo tofauti tofauti nchinij jambo ambalo limeibua dhana ya kufifisha nguvu ya kampeni kwa baadhi ya vyama.

Kufuatia hali hiyo Shirika la Umeme Nchini TANESCO limekanusha madai ya kukata umeme kwa makusudi ili kuhujumu kampeni za uchaguzi kwa baadhi ya vyama vya upinzani zisionekane na kusikika kupitia vituo mbalimbali vya luninga na redio.

Akizungumza jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari Meneja Uhusiano wa shirika hilo Adrian Severin amesema kukatika kwa umeme huo kunatokana na mgao unaoendelea nchi nzima kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya gesi kwenda Gridi ya Taifa.
 

Aidha,Severin huyo amesema Tanesco inajiendesha kibiashara na haina mlengo wowote wa siasa hivyo kukatika kwa umeme ni sehemu ya mgao unaoendelea ili kupisha ujenzi wa mitambo hiyo ya gesi.

Mbali na hayo, Severin amesema kwa muda mrefu Watanzani wamekuwa wakilalamikia tatizo la kukosa umeme wa uhakika hivyo amewataka kuwa wavumilivu wakati huu ambao kazi ya ujenzi inaendelea.
 

Hata hivyo imeelezwa kwamba kukamilika kwa ujenzi wa miundombinu ya gesi kwenye mitambo ya Kinyereza kutaongeza kiwango cha megawalt 200 zaidi katika gridi ya Taifa, hivyo kupunguza tatizo la umeme linaloendea nchini.

No comments:

Post a Comment