Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 12 September 2015

TCRA YAWAPIGA 'STOP' AMBAO SI WAGOMBEA WALA WAWAKILISHI WA VYAMA VYA SIASA KUONEKANA KWENYE VIPINDI VYA MOJA KWA MOJA VINAVYOHUSU SIASA

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imevitaka vituo vya utangazaji vyote nchini kutotoa nafasi kwa watu ambao si wagombea wala wawakilishi wa vyama, kushiriki vipindi vya moja kwa moja 'live' vinavyohusu shughuli za uchaguzi.

Katika taarifa yake jana, Mkurugenzi wa TCRA, Dk Ally Simba alisema kuanzia Septemba 10 mwaka huu katika kipindi chote cha kampeni za uchaguzi mkuu, watu ambao sio wagombea wa udiwani, ubunge, urais, wasemaji rasmi wa vyama au watu wasioteuliwa na vyama vya siasa kama wawakilishi, hawataruhusiwa kushiriki katika vipindi vya moja kwa moja vinavyohusu shughuli za uchaguzi vitakavyorushwa na vituo vya utangazaji.

Alisema utaratibu huo ni kwa mujibu wa kanuni za huduma za utangazaji (maudhui) na utangazaji wa uchaguzi wa vyama vya siasa (2015) na hasa katika kanuni ya 4 (f), (h), (i), 5 (b), (e) na (f).

Alisema hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya kituo cha utangazaji kitakachokwenda kinyume na utaratibu huo.

No comments:

Post a Comment