Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 24 September 2015

TEAM NZIMA YA MANDAI HERBALIST CLINIC INAKUPA UJUMBE HUU WA IDD EL HAJJ. SOMA HAPA


Habari za leo mdau wa www.dkmandai.com, leo ni Septemba 24, ambapo waamini wa dini ya kiislam kwa pamoja wanaungana kusheherekea sikukuu ya Idd El Hajj.

Kufuatia sikukuu hii Mandai Herbalist Clinic ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu Tabibu Abdallaha Mandai tunapenda kuwatakia sikukuu njema ya Idd El Hajj.

Lakini wakati tukiwatakia kheri ya sikukuu hii pia tunapenda kuwakumbusha wazazi kuwa makini na watoto katika siku hii, kwani siku kama ya leo mara nyingi watoto hupenda kutembea sehemu mbalimbali kwa lengo la kufurahi hivyo kuna haja ya wazazi kuhakikisha watoto wanapata uangalizi makini kwa siku hii.

Tunatambua kwamba watoto wengi siku hii ya leo hupenda kuogelea, hivyo ni vyema wazazi kuhakikisha watoto wanafika sehemu hizo wakiwa na uangalizi mzuri na wakutosha ili kuzuia maafa na kuifanya sherehe hii kuisha vizuri kwa amani na upendo.


Mbali na hayo Team nzima ya wafanyakazi ya Mandai Herbalist Clinic ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu Tabibu Abdallaha Mandai tunapenda kuwatakia siku njema na afya njema pia Watanzania wote na watu wote duniani kwa ujumla.

Unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment