Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 21 September 2015

UKIONA MABADILIKO HAYA MWILINI MWAKO NI VYEMA UONANE NA WTAALAM WA AFYA HARAKA


Kuna wakati miili yetu huwa tunahisi kuwa na hali ya tofauti na tulivyozoea, lakini huenda tukawa tunapuuza pale tunapokumbwa na hali hiyo.

Sasa leo napenda kukwambia haya mambo machache ambayo hupaswi kuyapuuza hata kidogo mara unapoona yametokea kwenye mwili wako.

Moja ya mambo ambayo hupaswi kuyapuuza kabisa ni endapo utahisi viungo vyako vya mwili vinakuwa dhaifu na kukosa nguvu kadri siku zinavyozidi kwenda. Endapo utaona hali hiyo ni vyema ukafanya jitihada za kuonana na wataalam kwani hali hiyo huweza kuwa ni kiashiria cha tatizo la kiharus 'stroke' hivyo ni vyema kutopuuza.

Dalili nyingine ambayo haipaswi kabisa kupuuza ni mara unapohisi maumivu ya kifua. endapo ukihisi hali ya maumivu hayo ya kifua kwa ndani inakupasa ufanye utaratibu wa kuonana na wataalam wa afya walio karibu na wewe na uelezee hali hiyo.

Hali hii ya maumivu ya kifua si ya kupuuza kwani huweza kuwa ni kiashiria cha magonjwa ya moyo au shambulio la moyo.

Tatizo jingine ambalo unapaswa kuogopa ukiliona ni hili la kupata haja ndogo (mkojo) wenye mchanganyiko wa damu. Ikiwa unapata hajandogo ya namna hiyo na yenye kuambatana na maumivu makali ya mgongo hali hiyo huashiria tatizo la mawe kwenye figo.

Pia kama unapata haja ndogo yenye damu bila kuhisi maumivu yoyote hiyo nayo huashiria saratani ya figo au kibofu cha mkojo, hivyo unashauriwa kuwaona madaktari mara moja.

Hali ya mapigo ya moyo kwenda kasi nayo ni hali mbaya ambayo unapaswa kuchukua hatua unapokumbwa na hali hiyo, hali hii huweza kuwa ni kutokana na tatizo la pumu 'athma' au magonjwa ya mapafu, lakini pia huweza kuwa ni tatizo la mzio 'allergy'

Jambo jingine ambalo hupaswi kulipuuza ni pale unapohisi kuzongwa na hali ya kuwa na mawazo ya kujiua. Unapoona unazongwa na mawazo ya namna hii unatakiwa kufanya jitihada za kuonana na wataalam wa maswala ya afya ya akili na saikolojia ili kukusaidia katika hilo.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment