Tuesday, 22 September 2015

UNAPOKUMBWA NA KIKOHOZI FANYA HAYA YAFUATAYO

Kukohoa ni mojawapo ya njia ya kusafisha koo baadhi ya vitu ambavyo huweza kumfanya mtu kujisikia kutokuwa na amani kwenye koo lake, sasa pale anapokohoa ni kama anasafisha.

Lakini kukohoa pia huweza kusababishwa na maambukizi kwenye njia ya mfumo  wa hewa hapo ndipo sasa huwa tunasema mtu amepatwa na shida, huenda akawa anakohoa kwa sababu ya tatizo ya mzio au allergy ya baadhi ya vitu fulani fulani,

Moja ya dawa nzuri ya kukabiliana na shida hii ni matumizi ya asali na juisi ya limao, mtu mwenye tatizo la kukohoa mara kwa mara anashauriwa kupata mchanganyiko wa asali na limao kidogo ili kuondosha tatizo hilo.

Hata hivyo, endapo mhusika atakuwa anakohoa mara kwa mara kwa muda wa wiki mbili hadi tatu mfululizo basi inashauriwa mhusika afike kwenye kituo cha afya kwa ajili ya vipimo zaidi ili kuweza kubaini endapo amepata maambukizi ya kifua kikuu na kuweza kuanza matibabu rasmi.

Tafadhari endapo ukihitaji kutumia tiba hiyo ya asali na juisi ya malimao kama ni tiba ni vyema ukapata ushauri kwanza kwetu kupitia simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com. Epuka kutumia tiba hii pasipo kupata maelekezo kutoka kwa wataalam


No comments:

Post a Comment