Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 26 September 2015

UNAWEZA KUVIFAHAMU VIASHIRIA VYA MAGONJWA YA NGONO KWA WANAUME KWA DALILI HIZI

Kwa kawaida wanaume wanapopatwa na magonjwa ya ngono huwa ni ngumu kidogo kuanza kuzishuhudia dalili za magonjwahayo tofauti na ilivyo kwa wanawake ambao wao huanza kuona dalili za tatizo mapema zaidi.

Sasa leo napenda kuziweka wazi hizi dalili ambazo hujitokeza kwa wanaume pale wanapopatwa na maambukizi ya magonjwa ya ngono.

Dalili za magonjwa ya ngono kwa wanaume / wavulana ni pamoja na:

- Jeraha, vidonda, upele au malengelenge juu au karibu na uume

- Kutokwa vitu kama usaha kwenye uume

- Maumivu au hali kama kuwashwa wakati wa kukojoa

- Maumivu wakati wa kufanya ngono

- Maumivu na uvimbe wa korodani

- Uvimbe wenye ukuaji usio wa kawaida kwenye sehemu za siri

- Vipele, ikiwa ni pamoja vipele katika kiganja cha mkono,nyayo za miguu.

Kama wewe au mpenzi wako ana dalili yoyote kati ya hizi ni muhimu kwenda zahanati au hospitali iliyokaribu nawe ili uweze kufanyiwa vipimo na kupata matibabu zaidi.

Pia unaweza kuwasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kutoka Mandai Herbalist Clinic kwa ushauri zaidi piga simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment