Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 21 September 2015

VIFAHAMU HIVI VYAKULA AMBAVYO VITAIMARISHA KINGA ZAKO ZA MWILI HADI UTASHANGAA MWENYEWE

Wheat Germ in Bowl
Habari za Jumatatu hii mdau wangu wa www.dkmandai.com sina shaka utakuwa upo vyema, lakini kama hali ni tofauti na matarajio yangu napenda kutoa pole kwako.

Jumatatu hii nimeona ni vyema tufahamu baadhi ya vyakula ambavyo huweza kuimarisha kinga za mwili, hii ni kwa sababu siku zote waswalihi tunasema kinga ni bora kuliko tiba.

Siku zote mtu mwenye kinga imara huwa ni nadra sana kusikia akisumbuliwa na magonjwa mbalimbali mara kwa mara.

Sasa kama na wewe unapenda kuwa na kinga imara ili usipate kuandamwa na magonjwa mara kwa mara inabidi uzingatie kutumia vyakula vifuatavyo:
Savoy Cabbage

Kabeji ni mojawapo kati ya mboga zenye uwezo mzuri sana wa kuimarisha kinga za mwili na kuzifanya kuwa na uwezo wa kupambana na madui vizuri mwilini. Iwapo utaweza ni vyema ukiandaa supu yake ukawa unakunywa angalau kwa wiki mara mbili hadi mara tatu.


Maziwa mtindi nayo ni sehemu pia ya kufanya kinga za mwili kuwa imara, unaambiwa kupata glasi moja ya maziwa mtindi kila siku hutosha kabisa kuimarisha kinga zako za mwili kuweza kupambana na magonjwa.

Kitunguu swaumu nacho kipo kwenye orodha hii ya vitu vyenye kuimarisha kinga za mwili na hii ni kutokana na kuwa na kirutubisho kiitwacho antioxidants ambacho husaidia kuimarisha kinga za mwili. Miongoni mwa bacteria ambao upigwa vita sana na kitunguu swaumu ni pamoja na bacteria wa H.pylori ambao huchangia matatizo ya vidonda vya tumbo na saratani ya tumbo.Fresh Spinach Leaves in Bowl

Spinachi nayo haikuwekwa kando katika 'list' hii kwani mboga hii ya majani ni chanzo cha 'folate' kirutubisho ambacho husaidia utengenezwaji wa seli mpya mwilini, lakini pia mboga hii ina kiwango cha nyuzinyuzi 'fiber' pamoja na vitamin C.Sliced Raw Yam


Viazi vitamu navyo husaidia sana kuongeza uimara wa kinga za mwili kutokana na kuwa na antioxidants pamoja na vitamini A ambayo humpunguzia mhusika nafasi ya kukupwa na matatizo ya saratani.
Slice of Watermelon


Tikiti maji nalo ni kinara wa kuwezesha mwili kuwa na kinga imara na hivyo kuufanya mwili kuweza kuwa na afya bora na kushindwa kupata maambukizi kirahisi.

Pamoja na hayo ngano pia nayo inaingia kwenye orodha ya vile vitu vyenye uwezo wa kuimarisha kinga za mwili.

Ikiwa utahitaji ushauri wa kimatibabu au kuna ugonjwa unakusumbua basi usisite kuwasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com au fika Mandai Herbalist Clinic iliyopo Ukonga, Mombasa maeneo ya Mongolandege jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment