Friday, 11 September 2015

WAANGALIZI WA UCHAGUZI MKUU WAPEWA MUONGOZO

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe, akizungumza na Mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini, kuhusu nafasi na majukumu yao katika uchaguzi mkuu, pamoja na jinsi Serikali ilivyojipanga kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa amani, huru na haki kwa vyama vyote.
Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, imesema kuwa waangalizi wa Uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu, hawatakiwi kutoa tamko lololote kuhusiana na uchaguzi au kampeni kabla ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutangaza matokeo.
Waziri husika wa Wizara hiyo, Mh Bernard Membe amesema hayo wakati akizungumza na Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini Tanzania, ambapo amesema waangalizi hao wanaweza kutoa ripoti zao baada ya kuthibitishwa na Wizara hiyo au NEC na ZEC.

Aidha, amesema kuwa waangalizi wote watakuwa huru kufanya kazi zao na serikali itahakikisha wanakuwa salama kwa muda wote watakapokuwa hapa nchini, huku akiwaeleza kuwa hawataruhusiwa kufika katika baadhi ya maeneo yatakayoainishwa Tume ya Uchaguzi.


 CHANZO: WAVUTI

No comments:

Post a Comment