Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 10 September 2015

WALEMAVU WA MACHO WATAPIGA KURA WENYEWE UCHAGUZI MKUU MWAKA HUU

Imeelezwa kwamba kwa mara ya kwanza nchini (Tanzania), watu wenye ulemavu wa macho watashiriki katika kumchagua kiongozi wanayemtaka kwa kutumia kifaa maalum chenye maandishi ya nukta nundu au 'Braille' katika uchaguzi mkuu utakofanyika Oktoba 25 mwaka huu.

Taarifa zinasema kuwa vifaa hivyo vitaanza kufanyiwa majaribio mwishoni mwa mwezi huu ambapo watu hao wataweza kufundishwa jinsi ya kupiga kura bila ya kuwa na mtu wa kumsaidia au kumwongoza kupiga.

Hatua hii inafuatiwa baada ya kuwepo na madai kuwa wale waliokuwa wakiwasaidia watu wenye ulemavu wa kuona mara nyingi huwapotosha walemavu hao kwa kupiga kura kinyume ya matarajio ya mlemavu husika.
 

Miaka yote ya nyuma walemavu wa macho wamekuwa wakishiriki katika kupiga kura kwa kusaidiwa na watu ambao huwa wanaenda nao katika vituo vya kupigia kura kwa lengo la kuwaelekeza wakati mwingine husaidiwa na mawakala au wasimamizi wa vituo vya kupigia kura.

CHANZO: BBC SWAHILI

No comments:

Post a Comment