Sunday, 13 September 2015

WIZARA YA MAMBO YA NJE IMETOA TAARIFA HII KUHUSU WATANZANIA WALIOKUWA MECCA BAADA YA AJALI YA MSIKITI

Moja ya taarifa kubwa zilizosikika sana duniani September 12, 2015 ilikuwa ni kuhusu kuanguka kwa winch ya kujengea ambayo ilikuwa inatumika kwenye ujenzi wa eneo la pembeni ya msikiti mtakatifu wa Mecca, uliopo Saudi Arabia ambako waumini wengi wa dini ya Kiislamu huwa wanakwenda kwa ajili ya Hijjah.

Ninayo taarifa rasmi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambayo inahusu hali ya Watanzania ambao wako Mecca kwa ajili ya Hijjah… Taarifa hiyo inasema hakuna Mtanzania yoyote ambaye amejeruhiwa wala kuumia kutokana na ajali hiyo.


Ipitie mwenyewe taarifa hiyo hapo chini>>>>>
Hijjah
Hata hivyo, idadi ya watu waliofariki ni 107 na wengine 200 wamepata majeraha>> MWENYEZI MUNGU awapumzishe kwa amani wote waliofariki na awape nafuu pia wote waliopata majeraha kwenye ajali hiyo.

No comments:

Post a Comment