Tuesday, 29 September 2015

YAFAHAMU MAMBO 9 AMBAYO YATAKUSAIDIA KUEPUKA MAGONJWA YA NGONO

Vijana ni kundi ambalo liko katika hatari zaidi ya kupata maambukizi ya magonjwa ya ngono kutokana na kuwa na hisia kali za kupenda na pia hamu ya kufanya tendo la kujamiana hujitokeza kwa nguvu kutokana na kukua.

Hali hiyo huchochewa na vichocheo / homoni vilivyomo ndani ya mwilini ambavyo katika kupanda na kushuka husababisha hisia za kufanya tendo la kujamiiana.

Hivyo basi vijana ni moja ya kundi ambalo endapo watakosa ufahamu wa kutosha kuhusu miili yao wanaweza kujiingiza katika tabia hatarishi za kujamiana hovyo pasipo kuchukuwa tahadhari ya kupata magonjwa ya ngono.

Mandai Herbal Clinic kwa kutambua kuwa vijana ndio nguvu kazi ya taifa lolote tumeona ni vyema leo tukafahamishana hizi mbinu za kupambana na magonjwa ya ngono kwa vijana:
Ili kuepukana na maambukizi ya magonjwa ya ngono zingatia yafuatayo

1. Kuepuka kujihusiha katika mauhusiano wakati wa umri mdogo

2. Acha ulevi au matumizi ya madawa ya kulevya kwani vyote hivyo huweza kuleta vishawishi vya matendo ya ushiriki ngono tena zisizo salama.

3. Jiepushe na vitendo vya ubakaji

4. Jihadhari kukutanisha ndimi (denda) ‘romance’ naa mtu usiyejua hali yake ya afya

5. Epuka kushiriki mapenzi ya mdomo kwa kunyonya uume au uke wa mwenza wako.

6. Jaribu kutumia muda mwingi kufanya kazi, kusoma au sanaa

7. Ogopa kuwa na ukaribu na makundi ya vijana walevi , wazurulaji na wavuta bangi au watumiaji wa madawa ya kulevya

8. Epuka vishawishi kama zawadi kutoka kwa watu usiowafahamu vizuri, pamoja na lifti za magari barabarani.

9. Tumia kondomu ya kiume au ya kike kwa usahihi zaidi kila tendo moja la kujamiana

Kama unahitaji ushauri zaidi au unasumbuliwa na magonjwa mbalimbali yakiwemo magonjwa ya ngono basi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment