Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 4 September 2015

YAPATE HAPA MASWALI MATATU MUHIMU YALIYOULIZWA LEO KWA TABIBU MANDAI NA MAJIBU YAKE

Tabibu Aballaha Mandai

Leo Septemba 04, 2015 Tabibu Mandai alikuwa live kupitia kipindi cha 'Hatua 3' kinachoruka kupitia Times Fm iliyopo Kawe Beach jijini Dar es Salaam.

Tabibu Mandai kupitia kipindi hicho alikuwa akijibu maswali ya wasikilizaji mbalimbali juu ya matatizo ya kiafya ambayo yanawatatiza, nimekukusanyia baadhi ya maswali yaliyoulizwa pamoja na majibu aliyojibu Tabibu Mandai.

Swali: Mimi shida yangu huwa napata michubuko sehemu za mapajani je, tatizo hili linasababishwa na nini?

Tabibu Mandai majibu: Kwa tatizo hilo kinachotakiwa ni kubadili utaratibu wa kuvaa mavazi ya kubana na badala yake kuvaa mavazi yenye kuachia mwili hasa zile sehemu za mapaja, lakini pia anaweza kutumia asali kwa kupaka zile sehemu zenye michubuko na anapaswa kupaka usiku wakati wa kuelekea kulala husaidia sana kumaliza shida ya hiyo michubuko.

Swali: Mimi ni kidume shida yangu nikwamba titi moja la kifua limekuwa kubwa je, tatizo hili linasababishwa na nini?

Tabibu Mandai majibu: Hiyo shida mara nyingi hutokana na tatizo la homoni, lakini ni vizuri kufanya utaratibu wa kuonana na wataalam kwa ajili ya kupata ushauri zaidi juu ya tatizo hilo.

Swali:Nina tatizo la kukosa hedhi ni mwaka wa tano sasa sijaona kabisa siku zangu, je hili ni tatizo?

Tabibu Mandai majibu: Kwanza kabisa ni kweli kukosa hedhi ni tatizo kwani kila mwanamke ambaye ameshafika umri unaofaa kupata siku zake huwa anapaswa kuzipata siku hizo kila mwezi, isipokuwa wale kinamama ambao wamefikisha umri wa kufunga hedhi (menopause) ambayo huwa mara nyingi ni kuanzia miaka 45 na kuendelea, hivyo kama mwanamke hapati hedhi basi huwa kuna shida hapo maana kupata zile siku pekee yake pia ni moja ya kudhihirisha afya kuwa njema kwa mwanamke .

Lakini pia kukosa hedhi kwa kipindi kirefu kama  hicho huweza kusababishwa na mabadiliko au mvurugiko wa mfumo wa homoni au mirija ya uzazi inapotokea kuziba, lakini pia hata wale ambao wana historia ya kutoa mimba huko nyuma huweza kukumbwa na tatizo hilo.

Hayo ndiyo baadhi ya maswali machache tu ambayo Tabibu Mandai aliulizwa na wasikilizaji wa kipindi cha Hatua 3 leo asubuhi majira ya saa 5 kuelekea saa sita hivi na hivyo ndivyo alivyoyajibu, lakini pia nawe unaweza kuendelea kumuuliza maswali yako Tabibu Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com


No comments:

Post a Comment