Thursday, 10 September 2015

ZIFAHAMU HIZI FAIDA ZA VYAKULA VYENYE ASILI YA MIZIZI

Vyakula vyenye asili ni miongoni mwa vyakula ambavyo vimekuwa vikionekana kusaulika sana na baadhi ya familia nyingi hapa nchini na tunapozungumzia vyakula vya mizizi basi tunahusisha viazi, mihogo, magimbi n.k

Pamoja na kuonekana kusaulika huko kwa vyakula hivyo, lakini bado ukweli utabaki kwamba vyakula hivyo ni miongoni mwa  vyakula muhimu sana kwa afya zetu.

Vyakula vyenye asili ya mizizi vinasifika sana kwa kuongeza nguvu mwilini kutokana na kuwa na kiwango kizuri na cha kutosha cha wanga.
Mihogo
Aidha, vyakula hivyo pia vinasifika kwa kuwa na kiwango kingi cha nyuzinyuzi yaani 'fiber' ambazo husaidia sana kurahisisha umeng'enyaji wa chakula tumboni.
Magimbi
Pamoja na maelezo hayo, lakini hapa ninayo sauti ya Tabibu Abdallaha Mandai kutoka Mandai Herbalist Clinic akielezea kwa uzuri zaidi umuhimu wa matumizi ya vyakula hivyo vya mizizi, Karibu umsikilize hapa chini bonyeza play>> >>>
Kwa maelezo zaidi wasiliana na Tabibu Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.co.

No comments:

Post a Comment