Wednesday, 16 September 2015

ZIPATA HIZI FAIDA ZA KABICHI, HUENDA UKAANZA KUIPENDA LEO MBOGA HII


Wengi tunaifahamu kabichi kama mboga. lakini huenda baadhi yetu hatuna ufahamu mzuri kuhusu mboga hii kama nayo inaweza kutumika kama tiba.

Kuna faidi lukuki za kabichi ikiwa ni pamoja na kupunguza unene, na sifa hiyo inatokana na mboga hiyo kuwa na kalori ndogo ilizonazo na ufumwele wingi.

Aidha, kabichi pia huweza kumsaidia mtu kuukinga mwili dhidi ya magonjwa hatari ikiwemo saratani. uwezo huo wa kabichi ni kutokana na kiasi kikubwa cha aina tatu muhimu za 'Antioxidant', 'Anti-inflammatory' na 'Glucosinolates,' ambazo zina uwezo wa kudhibiti magonjwa kadhaa nyemelezi yanayosababisha saratani za aina mbalimbali mwilini.

Hivyo kutokana na madhara na mateso yatokanayo na ugonjwa wa saratani, na kwa kuzingatia upatikanaji wa kabichi usiokuwa na gharama, huna sababu ya kupuuza ulaji wake.

Kabichi pia ni mboga yenye kiwango cha kutosha cha aina mbalimbali za vitamin hasa vitamini K, B1, B2, vitamin A na C. Aidha, kabichi ina kiasi kingi cha ufumwele au kamba lishe kwa maana ya fiber, ambapo vyote hivyo ni kinga ya mwili dhidi ya magonjwa nyemelezi.


Kabichi inakinga ugonjwa huu wa saratani, hususani inapotumika juisi yake. Miongoni mwa faida za juisi hizo ni ni kusaidia usagaji mzuri wa chakula.

Unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment