Thursday, 1 October 2015

BAADHI YA MAHUJAJI KUTOKA MECCA SAUDIA ARABIA WAANZA KUWASILI TANZANIA

September 24,  2015 zilitolewa taarifa za kuhusu watu zaidi ya 700 kufariki kwenye Msikiti Mkuu ambao Waumini wa Dini ya Kiislamu huenda kwa ajili ya Hijjah uko Sudia Arabia, Mecca.

Sasa jana Septemba 30, 2015 kiongozi wa dini ya Kiislamu, Hemed Jalala alikutana na waandishi wa habari na mara baada ya kurejea nchini na kuzungumzia yaliyojiri.

Jalala alisema "Kwa kuwa leo ndio tumefika (jana) Tanzania tukitokea katika misafara inayotoka kule Hijjah Saudi Arabia naamini kuna watu watakuwa wanataka kufahamu kilichotokea kule Saudi Arabia, ningependa kusema kwamba tunamshukuru tumemaliza ibada hii ya Hijjah katika hali ya usalama sisi kama watanzania, lakini jambo la kusikitisha na la kuliza ni kwamba hatukurudi sote ambao tumekwenda kutekeleza ibada hiyo"

Aidha, Hemed Jalala alisema pamoja na kutekelza ibada hiyo, lakini kilichotokea mwaka huu ni jambo la kusikitisha kwani idadi ya watu waliokufa ni wengi mno.

"Watu waliokufa ni wengi mno na tukizungumzia ripoti za mwisho ni idadi ya watu 4000 kwa hiyo tumewakosa watu ambao walikuwa wakipiga mawe saba kwenye nguzo yaani kumpiga sheta huku njia mbili zikiwa zimefungwa na hapo ndipo watu walipoanza kupoteza maisha"  Hemed Jalala.

Mbali na hayo Hemed Jalala ameitumia lawama Serikali ya Saudi Arabia kufuatia tukio la vifo hivyo.

"Sisi na nikiwemo kama Imamu wa msikiti wa Kigogo na moja wa viongozi wa Dini kwakweli tunaibebesha serikali ya Saudi Arabia kwa uzembe uliotendeka na uliofanyika katika tukio hilo, kwanini linabeba kwanza ziko barabara kubwa ambazo hazipungui mita 300 kwanini mahujaji hawakuruhusiwa kupita katika barabara zile, la pili sehemu na hili ni muhimu vilevile sehemu ile iliyokuwa imezungukwa na camera nyingi hivi zile camera zilikuwa haziona tukio hili linaloendelea kwa hiyo huo ni uzembe uliojitokeza katika Ardhi ya Mecca ili limebebwa na serikali na wenyewe wamekubali" alisema Hemed Jalala

No comments:

Post a Comment