Friday, 30 October 2015

FAHAMU KAMA UNAZO DALILI ZA KUKOSA MTOTO NA UPATE SULUHISHO HAPA


Habari za leo Ijumaa mdau wangu wa www.dkmandai.com ninayofuraha kukukaribisha kwenye muendelezo wetu wa kufahamishana  taarifa mbalimbali hususani za afya, hapa leo ninazo dalili zinazoashiria mwanamke kushindwa kushika ujauzito. Karibu

Tatizo la kushindwa kushika ujauzito kwa mwanamke husumbua familia nyingi na husababishwa na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na tatizo upande wa wanaume.

Familia nyingi au wanandoa wengi huanza kuhisi tatizo baada ya kuishi katika mahusiano ya kutafuta ujauzito kwa zaidi ya mwaka mmoja lakini hakuna mafanikio.

Ili mwanamke apate mimba ni lazima awe na sifa za kupata ujauzito, na ili mwanaume aweze kumpa mwanamke mimba ni lazima awe na sifa za kumpa mwanamke mimba, hivyo utaona kwamba matatizo haya huweza kuwepo kwa pande zote mbili au mojawapo.

Kutokana na kwamba tatizo hili huwahusu wanandoa wote wawili yaani mwanamke na mwanaume hivyo ni vyema wakati wa utafutaji wa ujauzito mwanamke na mwanaume wote kwa pamoja wakashirikiana kwani mwanaume unaweza kujiona huna tatizo kumbe ukija kupima mbegu zako utajikuta unatatizo kubwa.

Matatizo kwa upande wa mwanamke
Mwanamke mwenye tatizo la kutopata ujauzito anaweza kuwa na mojawapo ya matatizo haya yafuatayo;

Atakuwa amekaa na mume au yupo katika mahusiano ya kutafuta mtoto kwa zaidi ya mwaka lakini hakuna mafanikio, pia huweza kuwa analalamika maumivu ya chini ya tumbo mara kwa mara au yanaweza yasiwepo.

Lakini pia mwanamke mwenye tatizo la kutoshika ujauzito huweza kuwa na maumivu ya hedhi, kuvurugika kwa mzunguko na kutoona ute wa uzazi. hizo huweza kuwa moja ya viashiria vya tatizo hilo.

Pamoja na hayo pia wanawake wengi wenye shida hii ni nadra sana kuwa na hamu ya tendo la ndoa au kutojihisi raha wakati wa tendo na huhisi maumivu wakati wa tendo au kutokwa na uchafu ukeni wakati mwingine huambatana na muwasho na harufu.

Dalili nyinngine ya tatizo hili la kushindwa kushika ujauzito ni pamoja na kuwa na historia ya kuharibu au kutoka kwa mimba, historia ya kuzaa, au kufanyiwa upasuaji wa aidha uzazi au mirija. Ingawa wengine hawana historia hizi.

Endapo utahisi una matatizo ya kutopata ujauzito na unazo dalili hizo hapo juu au huna, basi ni vizuri kuonana na daktari wa magonjwa ya matatizo ya uzazi katika hospitali za mikoa. Uchunguzi utafanyika kuangalia mfumo wako wa homoni au vichocheo vya uzazi, vipimo vya kizazi na mirija na vingine ambavyo daktari atashauri. Au wasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment