Friday, 2 October 2015

FAHAMU KUHUSU TATIZO LA KUPATWA MAUMIVU YA VIUNGO NA NAMNA YA KUJITIBU KWA KUTUMIA TIBA ASILI

Baridi yabisi au (maumivu ya viungo)ni ile hali ya mchocheo wa maumivu (inflamation) ndani ya misuri na maungio mbalimbali ndani ya mwili.

Mara nyingi huwa ni ngumu kidogo kutofautisha kati ya baridi yabisi na jongo 'gout'

Kimsingi ni kwamba baridi yabisi inapokosa kutibiwa mapema huweza kumlemaza mgonjwa na mbaya zaidi ugonjwa huu huweza kumpata mtu yeyote.

Kuna wakati ambapo utumbo mkubwa hushindwa kunyonya chumvi  za muhimu katika mzunguko wa damu hali hiyo huweza kusababisha upungufu wa chumvi iitwayo soda fasteti (phosphete of soda) ndani ya chembechembe za mwili husababisha ugonjwa wa baridi yabisi.

Ili kupunguza makali ya tatizo hili mgonjwa anaweza kutumia limao, ambapo atatkiwa kupata juisi yake angalau kila siku nusu glasi hadi pale atakapoona mabadiliko au unaweza kutumia kitunguu swaumu ambapo atatakiwa kula punje za kitunguu swaumu kila siku 3, hii ni kwa sababu kitunguu swaumu kina manufaa ya ziada ya mwili, utumiaji wa kitunguu swaumu utumike hadi pale utakapoona mabadiliko.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 barua pepe dkmandaitz@gmail.com


No comments:

Post a Comment