Tuesday, 6 October 2015

FAHAMU KUHUSU TATIZO LA UVIMBE KWENYE KIZAZI NA DALILI ZAKE ZOTE

Tunaposema uvimbe kwenye kizazi ni ile hali ya kuwa na uvimbe katika mfuko wa uzazi wa mwanamke ambao hujulikana kama 'fibroid'.

Uvimbe huo  hutokea kwenye misuli laini ya mfuko wa uzazi. Tatizo hili huwakumba wanawake wengi hususani wale wenye umri miaka 20 hadi 30 yaani wale ambao wapo katika umri wa kuzaa.

Tatizo hili mara nyingi huwa halioneshi dalili za wazi linapokuwa katika hatua za awali, lakini baadaye huanza kuonesha dalili.

Miongoni mwa dalili za tatizo hili ni pamoja na kutokwa damu nyingi kwa muda mrefu wakati wa hedhi ikiambatana na mabonge mabonge isivyo kawaida.

Dalili nyingine ni kutokwa damu isiyo ya kawaida katikati ya mwezi au hedhi zisizokuwa na mpangilio maalum.

Pia mhusika wa tatizo hili huweze kuhisi maumivu ya kiuno hasa wakati wa hedhi, laikini pia huambatana na maumivu makali ya tumbo.

Hali ya uvimbe kwenye kizazi pia huweza kusababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa na kukojoa mara kwa mara kwani uvimbe hukandamiza kibofu cha mkojo.

Dalili nyingi za tataizo hili ni historia ya kuharibika na kutoka kwa mimba mara kwa mara.

Halikadhalika tatizo lauvimbe kwenye kizazi husababisha ugumu wa kupata mtoto kwani uvimbe huo unapokuwa sana hukandamiza mirija ya kupitisha mayai kutoka kwenye ovari au sehemu mayai yanapotengenezwa, lakini pia huweza kuzuia yai lililorutubishwa kujishikiza kwenye kizazi.

Kama wewe ni mmoja wa wanaosumbuliwa na tatizo hili ni vyema ukawasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment