Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 20 October 2015

FAHAMU LEO KUHUSU SABABU ZITAKAZOKUFANYA UPATE UGONJWA TEZI YA SHINGO (GOITER)


Je, unafahamu kuhusu ugonjwa wa goita, hili ni jina ambalo hutumika kuwakilisha tatizo la kuvimba kwa tezi ya 'thyroid' ambayo hujitokeza eneo la shingoni.

Kiufasaha huu ugonjwa huu huonekana ukiwakuta zaidi wanawake hasa wale wanawake wasiopata muda wa kutosha wa kupumzika na kupata utulivu kuliko wanaume .

Dalili za ugonjwa huu ni kuwa na huzuni,  kupoteza uwezo wa kuzingatia mambo, lakini pia mgonjwa wa tatizo hili huwa ni mwepesi wa kukwazika mapema.

Dalili nyingine ni kuvimba kwa tezi ya shingoni na dalili hizi pia huambatana na hisia za uchovu uliopitiliza  na kutetemeka kwa mikono pamoja na ukosefu wa nguvu za misuli mwilini.

Kupungua kwa uzito pia ni dalili za tatizo hili ambazo hujitokeza kwa wale wanaoumwa ugonjwa huu na huweza kudumu kwa kipindi fulani cha tatizo hilo.

Chanzo cha ugonjwa huu ni ukosefu wa madini joto katika vyakula na kutoke kwa maudhi mengine yakihisia na kimwili 

Chanzo kingine ni kuwa na mazoea ya kula chakula kilichoondolewa uasilia wake na ambacho hakijapigwa, lakini pia chanzo kingine ni ulaji wa mara kwa mara wa vyakula vilivyopita kiwandani na vilivyoondolewa ladha halisi.

Miongoni mwa tiba za awali ni pamoja na mgonjwa kupata mapumziko ya kutosha na mara kwa mara, kufanya mazoezi, kula vyakula vyenye madini joto pamoja na kuondokana na mawazo.

Kwa maelezo zaidi au kuhusu tiba ya tatizo hili unaweza kuwasiliana na Tabibu Abadallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com. Karibu sana Mandai Herbalist Clinic kwa tiba ya magonjwa yote kwa kutumia mimea tiba tu.

No comments:

Post a Comment