Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 13 October 2015

HALI YA KIPINDUPINDU BADO JIJINI DAR ES SALAAM, IPATE HII RIPOTI KUHUSU HALI ILIVYO KINONDONI KWA SASA


Agosti 15, 2015 ndio ugonjwa wa kipindupindu ulianza kuripotiwa jijini Dar es Salaam, lakini ugonjwa huo umeonekana kutosikika sana huenda kutokana na vyombo vingi vya habari kujikita zaidi kuripoti ishu za kisiasa.

Sasa taarifa zilizopo ni kwamba ugonjwa huo bado upo jijini Dar es Salaam na watu wameendelea kupoteza maisha na wengine wameendelea kuambukizwa, huku wengine wakiwa bado wamelazwa na kuendelea kupata tiba hospitalini.

Kwa mujibu wa Afisa Afya wa Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam Mathias Kapizo amesema hali ilivyo katika manispaa hiyo kwa sasa ni "tuna wagonjwa wapya 35, wagonjwa 35 katika Wilaya kama Kinondoni ni watu wengi… Sehemu kubwa zilizoathiriwa na Kipindupindu kwa sasa ni Manzese, Tandale, Mabibo, Makurumla, Mburahati, Kigogo, Mwananyamala, Magomeni Sinza, Makumbusho na Kijitonyama.”

Kapizo aliongeza kuwa  “bahati mbaya tumepoteza watu 12 mpaka sasa kwa ugonjwa wa Kipindupindu… Kwa mujibu wa taarifa ya tarehe 12 jumla ya wagonjwa wote waliougua kipindupindu tangu kilipoanza tarehe 15 mwezi wa nane wanafikia 1564 kwa sasa"

Kuhusu idadi ya wagonjwa waliolazwa mpaka sasa, Mathias Kapizo amesema “Kwa takwimu za leo (Octoba 12)  katika wodi ya Makurumla tulikuwa na mgonjwa mmoja, Ubungo wagonjwa wawili, Mwananyamala wagonjwa watatu, Magomeni mgonjwa mmoja, Kawe wagonjwa wawili, Manzese wagonjwa watano, Tandale wagonjwa wawili, Sinza wagonjwa watano, Makongo mgonjwa mmoja, Mburahati wagonjwa sita, Kigogo wagonjwa wawili, Mbezi mgonjwa mmoja, kutoka Mlandizi wamekuja wagonjwa wawili, Wazo (Tegeta) mgonjwa mmoja, Makuburi mgonjwa mmoja, Kimara mgonjwa mmoja, Mabibo mgonjwa mmoja na Tabata mgonjwa mmoja."

Shukrani : Millard ayo.com

No comments:

Post a Comment