Tuesday, 20 October 2015

HAWA NDIO WATANZANIA WATAKAO AMUA HATIMA YA TANZANIA JUMAPILI HII OKTOBA 25Ikiwa zimebaki siku 5 kuelekea siku ya kupiga kura Oktoba 25, Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania imetoa takwimu kuhusu wapiga kura wanaotarajiwa kushiriki uchaguzi mkuu huo siku ya Jumapili.


Takwimu hizo zinaonesha wapiga kura wanaume ni asilimia 47 na wanawake asilimia 53, ikiwa na maana kwamba wanawake ni wengi kushinda wanaume katika sajili ya kura, huku wapiga kura vijana walio na umri wa kati ya miaka 18 na 35 wakiwa ni asilimia 57 ya wapiga kura wote.


Wapiga kura walio na umri wa zaidi ya miaka 50 ni asilimia 18 pekee, hao wengine asilimia 25 wakiwa na umri wa kati ya miaka 36 na 50.

Idadi ya wapiga kura kwa mujibu wa mikoa
NaMkoaIdadi ya wapiga kura
1Arusha1,009,292
2Dar es Salaam2,775,295
3Dodoma1,071,383
4Geita887,982
5Iringa529,887
6Kagera1,051,681
7Kaskazini Pemba11,570
8Kaskazini Unguja9,601
9Katavi322,127
10Kigoma792,551
11Kilimanjaro800,349
12Kusini Pemba8,986
13Kusini Unguja5,077
14Lindi514,558
15Manyara678,586
16Mara892,741
17Mbeya1,397,653
18Mjini Magharibi12,948
19Morogoro1,271,951
20Mtwara728,981
21Mwanza1,448,884
22Njombe383,366
23Pwani697,533
24Rukwa459,573
25Ruvuma739,774
26Shinyanga773,273
27Simiyu718,777
28Singida648,897
29Tabora1,097,760
30Tanga1,009,753
JUMLA22,750,789
Eneo la Unguja lina wapiga kura 358,180 na Pemba 145,013, jumla ya wapiga kura visiwani Zanzibar ikiwa 503,193.

Kwa jumla, wapiga kura wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni 23,253,982.

No comments:

Post a Comment