Friday, 9 October 2015

HAYA NDIO MENGINE MAZURI KUHUSU FAIDA ZA NDIZI MWILINI
Wengi wetu tunafahamu kuhusu tunda la ndizi kutokana na umaarufu wake duniani maarufu, lakini huenda wachache ndio tukawa tunajua faida za tunda hilo.

Ndizi ina aina tatu za kipekee za sukari zijulikanazo kama Sucrose, Fractose na Glucose na pia ina kiasi kingi cha nyuzinyuzi yaani 'fibre' ambacho husaidia sana katika usagaji wa chakula tumboni. 

Kutokana na virutubisho hivyo tunda hilo linapata uwezo mkubwa wa kuimarisha nishati ya mwili, na hivyo kuusaidia mwili kupata nguvu za kutosha kwa mlaji.

Nishati sio kitu pekee ambacho hupatikana ndani ya ndizi bali tunda hili lina faida nyingi ikiwa ni pamoja na kuusaidia mwili kuzuia magonjwa na matatizo kadhaa.

Vilevile ndizi ni chakula kinachujulikana kama tiba asilia kwa matatizo mengi ya kiafya. Unapofananisha ndizi na apple, ndizi zina protini mara nne zaidi, sukari mara mbili, potassium mara tatu na vitamini A chuma mara tano zaidi.

Vilevile vitamini na madini nyinginezo hupatikana katika tunda hilo. Kwa kuwa na kiasi kikubwa cha chuma, ndizi husaidia kushajiisha uzalishwaji wa hemoglobin katika damu, na hivyo kusaidi kuondoa upungufu wa damu.

Ndizi pia ina kiwango cha juu sana cha potassium na kiasi kidogo cha chumvi,hivyo hulifanya tunda hilo lifae zaidi katika kupambana na shinikizo la damu. 

Pia ndizi hizo hizo huweza kusaidia mwili katika kuimarisha uwezo wake wa kufyonza calcium, na hivyo kuifanya mifupa kuwa imara. 

Ikiwa utang'atwa na mdudu, jaribu kusugua sehemu ya ndani ya ganda la ndizi pale ulipong'atwa. Kufanya hivyo husaidia kupunguza maumivu, uvimbe na kuwasha.

Kama ungependa kuwasiliana nasi tupigie kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment